Mfahamu mwanamke aliyewahi kuvunja rekodi ya kuwa na misuli mikubwa zaidi

Mfahamu mwanamke aliyewahi kuvunja rekodi ya kuwa na misuli mikubwa zaidi

Katika ulimwengu wa sasa vipaji vimekuwa vikiwainua watu wengi hasa kuwapatia fedha za kuendeshea maisha yao na hata kumpatia mtu umaarufu katika maeneo mbalimbali.

Yote hayo hujitokeza mara tu mtu akiamua kutumia kipaji chake vizuri na kuona fursa anazoweza kuzipata kupitia kipaji hicho.

Kama kawaida wapo watu wenye vipaji mbalimbali kama vile kuimba, kuigiza, kusuka na vinginevyo, wakati unaendelea kufikiria juu ya kipaji chako. Mfahamu mwanamke mtunisha misuli ambaye ana misuli mikubwa zaidi.

Mwanamke huyo anafahamika kwa jina la Nataliya Kuznetsova, raia wa Russia ambaye alianza kukuza msuli yake alipokuwa na umri wa miaka 14, inaelezwa kuwa kabla hajaanza kukuza misuli alikuwa na mwili mwembamba kabisa.

Katika harakati zake za kukuza mwili wake amejikuta akiishi maisha ya kufanya mazoezi mbalimbali huku akiwa anatumia vyakula vya kujenga mwili wake kuwa na nguvu.

Nataliya hutumia lishe maalum, na mlo wake ni wenye ‘protini’ nyingi kupita kiasi, hupendelea kula nyama, mayai, samaki, mboga za majani na vingine lakini pia, Nataliya hunywa vinywaji vyenye vitamini nyingi ili kuongeza nguvu zake.

Kutokana na mwili wake umempatia mafanikio mbalimbali kama vile kushinda tuzo kwenye mashindano mbalimbali ya ukubwa wa misuli.

Licha ya kuwa na mwili wenye kuhitaji mazoezi ya mara kwa mara Nataliya amebahatika kuolewa na Vladislav Kuznetsova, mumewe huyo ambaye ni mwalimu wa mazoezi na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.

Nataliya alizaliwa mwaka 1991, ana zaidi ya kilo 123, amekuwa akipendwa na kufuatiliwa na watu wengi kwenye mitandao yake ya kijamii kwani kwenye Instagram hadi sasa amefikisha wafuasi
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags