Mfahamu muigizaji aliyepata umaarufu kwa kupostiwa na jeshi la polisi

Mfahamu muigizaji aliyepata umaarufu kwa kupostiwa na jeshi la polisi

Watu husema umaarufu haulazimishi bali unajileta wenyewe, na linapokuja suala la umaarufu kila mmoja ana njia aliyotumia ili afahamike.

Wakati baadhi ya watu wakitumia mbinu mbalimbali kufahamika, mfahamu mwanamitindo na muigizaji maarufu ambaye wala hakulazimisha umaarufu, bali alipendwa na watu mara baada ya kukamatwa na polisi kwa makosa ya uhalifu na kutumia bunduki, na kisha picha yake kuchapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa jeshi la polisi wakitoa taarifa ya muhalifu huyo kukamatwa.

Si mwingine bali ni Jeremy Ray Meeks ambaye awali alikuwa wanachama wa kundi la kihalifu la street Crips gang, Mwaka 2014 wakati wa 'operesheni' ya kusaka na kukamata makundi ya kihalifu California, Idara ya Polisi ya Stockton ilimkamata Meeks na wenzake watatu.

Hivyo basi picha za zilichapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Idara ya Polisi ya Stockton kwa lengo la kutoa taarifa kwa jamii kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata wahalifu sugu wa kutumia silaha.

Ndani ya saa 24 tangu picha hizo zichapishwe kwenye ukurasa huo , picha ya Jeremy ilionekana kupendwa ilipata "likes" zaidi ya 15,000 na comments zaidi ya 3,700, huku nyingi zikiwa za wanawake wakidai kuwa wanavutiwa na sura yake.

Watumiaji wa Twitter(x) waliunda hashtag "#felonrushfriday" kwa heshima ya Jeremy jambo ambalo lilipelekea Msemaji wa Idara ya Polisi ya Stockton, Joe Silva, kukiri kuwa picha ya Jeremy imewafikia watu wengi kuliko picha yoyote tangu walipofungua ukurasa huo mwaka 2012.

Kesi yake ilisikilizwa Julai 2014, huku akiwa kwenye gereza la San Joaquin County, ndipo mama yake, alianzisha ukurasa wa #GoFundMe kutafuta pesa ya dhamana na kumlipa wakili wa utetezi.

Februari 5,2015, Jeremy alitiwa hatiani kwa kosa moja la kumiliki bunduki, alihukumiwa kifungo cha miezi 27 gerezani, alitumikia miezi 13 kifungo hicho, na kutolewa Machi 8,2016, kisha akaamriwa kutumikia muda uliyobaki nje ya gereza.

Baada ya kutoka makampuni mbalimbali ya fashion kama vile 'White Cross Management' yalianza kumpa mikataba minono kwa ajili ya kufanya naye kazi ya kutangaza mavazi yao, hakuishia hapo akaingia kwenye filamu.

Kati ya filamu alizocheza ni 'Secret Society', 'Dance for me', 'Dutch', 'Trigger' na nyingine nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags