Mfahamu bondia aliyepata ulemavu baada ya kupigwa ngumi kichogoni

Mfahamu bondia aliyepata ulemavu baada ya kupigwa ngumi kichogoni

Tazama maisha ya bondia kutoka nchini Marekani Prichard Colon Melendez, yalivyo badilika kwa sekunde chache baada ya kupigwa ngumi akiwa ulingoni, na kusababisha maisha yake kwa ujumla kubadilika.

Mnamo Oktoba 17, 2015, katika ukumbi wa Eagle Bank Arena, Virginia bondia huyo alicheza pambano na Williams kwa pambano la raundi 9.
Katikati ya pambano hilo bondia William alimpiga Colon ngumi nyuma ya kichogo, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mchezo huo wa ngumi.

Kitendo hicho kilimpa shida Colon baada ya kumaliza pambano hilo inadaiwa alianza kutapika na baadaye kukimbizwa hospitali.
Majibu ya hospitali yalieleza kuwa ngumi alizopigwa nyuma ya kichogo zilipasua fuvu la kichwa na kuvujisha damu ndani ya ubongo hadi kupelekea ulemavu wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags