Nahodha wa timu ya Argentina Lionel Messi amesimamishwa kucheza katika klabu yake ya Paris St-Germain (PSG) kwa wiki mbili baada ya kusafiri katika nchi ya Saudia Arabia bila ruhusa ya klabu hiyo.
Safari yake ilifuatia kushindwa kwa klabu hiyo ya Ufaransa walipokuwa wakicheza na Lorient siku ya Jumapili, ambapo Messi alicheza kipindi chote cha dakika 90 za mechi.
Messi hatafanya mazoezi wala kuichezea PSG katika kipindi cha kusimamishwa kwake. Inafahamika kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliomba ruhusa ya kusafiri ili kufanya kazi za kibiashara lakini alikataliwa.
Messi, ambaye pia alipigwa faini na klabu, ana kazi kama balozi wa utalii wa Saudi Arabia.
Makamu wa rais wa Barcelona Rafael Yuste alidai mwezi Machi kuwa klabu ya Uhispania inawasiliana na Messi kuhusu kurejea kwake katika Nou Camp.
Leave a Reply