Messi akabidhi tuzo ya Ballon D or kwenye makumbusho ya Barcelona

Messi akabidhi tuzo ya Ballon D or kwenye makumbusho ya Barcelona

Mchezaji wa ‘timu’ ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ameonesha kuwa uhusiano wake na ‘klabu’ yake ya zamani ya Barcelona hauwezi kuvunjika, baada ya kukabidhi Tuzo yake ya nane ya Ballon d'Or kwenye jumba la makumbusho la Barcelona FC.

Messi ambaye kwasasa anakipiga katika ‘klabu’ ya Inter Miami iliyoko nchini Marekani alianza kuichezea ‘timu’ ya Barcelona kuanzia 2004 hadi 2021. akicheza ‘mechi’ 781, kufunga mabao 676 na kutoa asisti 237.

Nahodha huyo wa Argentina alipata tuzo yake ya nane ya Ballon d'Or iliyovunja rekodi ya kuwa mchezaji aliyechukua Tuzo nyingi zaidi, zikitolewa Oktoba 2023 akiwapita washindani wake Erling Haaland na Kylian Mbappe.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags