‘Mechi’ iliyochezwa jana Jumanne ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kati ya Brazil na Argentina iliingia dosari baada ya kucheleweshwa kuanza na kuwafanya mashabiki kuanzisha vurugu katika uwanja wa Maracanã ulioko Rio de Janeiro nchini Brazil.
Inadaiwa kuwa ‘mechi’ hiyo ilichelewa na kuanzishwa takribani baada ya dakika 27. Ambapo kufuatia video zinazo-trend mitandaoni zinawaonesha maofisa usalama wa Brazil wakiwapiga mashabiki wa Argentina.
Jambo ambalo lilifanya nahodha wa ‘timu’ ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi kuchukuwa wachezaji wake na kurudi katika vyumba vya kubadilishia nguo na kurejea tena uwanjani baada ya kukaa kwa dakika 22.
‘Mechi’ hiyo ilitamatika kwa bao 1-0 huku ‘timu’ ya Taifa ya Argentina ikiondoka na alama tatu bao lililofungwa na Nicolas Otamendi.
Leave a Reply