Mbwa alamba dili kampuni ya magari

Mbwa alamba dili kampuni ya magari

Mbwa mmoja aliyetambulika kwa jina la #TucsonPrime, ambaye hakuwa na makazi maalumu amepata ‘dili’ la kuwa mfanyakazi katika kampuni ya kuuza magari ya #Hyundai iliyoko nchini #Brazil.

#Tucson hapo awali alikuwa akiitembelea Kampuni hiyo mara kwa mara ambapo aliwavutia wafanyakazi kwa tabia yake ndipo Mfanyabiashara wa magari Emerson Mariano akaamua kumuajiri na kumpatia kitambulisho kama muuzaji wa magari wa kipekee.

#Emerson alieleza kuwa aliamua kumpa kazi Mbwa huyo kutokana na mwenendo wa tabia yake na ukarimu aliyokuwa akiuonesha kwa wafanyakazi wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags