Ikiwa imepita wiki moja tangu wasanii Mbosso, Billnass na Whozu kufungiwa kujihusisha na kazi za muziki, kutokana na video ya Whozu ‘Ameyatimba’ kuwa na maudhui yanayokiuka maadili, hatimaye wasanii hao wamekaa kikao na Bodi ya Basata na kufikia maamuzi ya kuwataka wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi zao za Sanaa.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wake Mwana FA wamefanya kikao hicho na wasanii hao, ambapo Whozu anatakiwa kulipa faini ya tsh 5 milioni, na kushusha wimbo huo kweye digital platform zote, Billnass atatakiwa kulipa tsh 1 milioni na Mbosso tsh 3 milioni.
Ikumbukwe kuwa awali adhabu za wasanii hao zilikuwa Whozu alitakiwa kutofanya kazi za muziki kwa muda wa miezi sita, na kulipa faini ya milioni tatu huku Billnass na Mbosso wakiwa wametozwa faini ya shilingi milioni tatu kila mmoja na kufungiwa kutojihusisha na kazi za Sanaa kwa muda wa miezi mitatu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply