Mbosso awajia juu waandaaji Tuzo za Muziki

Mbosso awajia juu waandaaji Tuzo za Muziki

Na Asha Charles

Alooooo! Tuzo za TMA zimezua balaa kwa baadhi ya wasanii kutoa mapovu kutokutajwa katika listi ya tuzo hizo ambapo mmojawapo akiwa ni msanii kutoka lebo ya WCB. Mbosso amewalalamikia waandaaji wa tuzo hizo kwa kile alichokiita kutokufanya kitendo cha kiungwana.

Tanzania Music Awards (TMA) siku ya jana Alhamisi ilitoa rasmi orodha ya wasanii watakaowania tuzo mbalimbali, basi bwana kwa msanii Mbosso kwake listi hiyo ilikuja tofauti na alivyotarajia ambapo amemaindi baadhi ya nyimbo zake kali kutokuwepo katika vingele hivyo vya tuzo.

Kupitia Instastory yake, Mbosso ameeleza kuwa “KHAN EP ilikuwa na kigezo gani cha kutokuwepo ALBUM/ EP halafu mniambie zilizokuwepo zimetoa hit ngapi labda, maana Khan Ep imetoa Shetani, Yataniua, Huyu Hapa, Assalam n.k” huku akidai kuwa kamati ya tuzo TMA inaendekeza chuki na roho mbaya.

Kutokana na baadhi ya wasanii kumwaga lawama zao kwa Baraza la Sanaa la Taifa Basata na Tuzo za TMA, imesema kuwa haihusiki na kumchagua msanii yeyote kipengele cha kuwania katika tuzo hizo.

Mbali na hayo  wamesema kwamba mpaka sasa haiwezekani msanii yeyote kuondolewa katika mfumo hivyo kila mwanamuziki ataendelea kujitangaza ili apate kura za kutosha kuanzia April 8-28, 2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags