Hellow!! Its another day, kama kawa kama dawa kwenye kipengele chetu pendwa kabisa cha masuala ya fashion hapa ndiyo sehemu ya pekee ya kujidai kwa wote wanaopenda urembo bwana.
Yees sifa moja wapo ya mwanamke lazima ume mrembo, usikose mvuto bwana au vipi, leo kwenye fashion nimekusogezea mbinu za kuandaa rasta zako kabla hujasogea kwa msusi ulikua unazifahamu mbinu hizo?twende sawa hapa.
Wengi wetu hua tukihitaji kusuka hususan rasta hua tunanua kisha tunakimbilia kwa msusi je unajua udambuudambu wa kuandaa kabla fuatilia dondoo hii ya kibabe mtu wangu.
Fahamu kuwa Asilimia kubwa ya wanawake kwa sasa wanasukia rasta, ni namna moja ya ku-protect nywele zako asilia lakini pia kuonekana mtanashati.
Mara nyingi baada ya kusikia rasta tunapatwa miwasho, hii ni kutokana na kemikali zilizopo katika rasta hizo tulizosukia. Lakini unaweza kuepukana na hali hii endapo tu utaziandaa kwa kuziosha rasta zako kabla ya kuzisukia.
Vifaa vya kuwa navyo pindi unapotaka kusafisha rasta zako.
- Apple Cider Vinegar
- Maji Ya Moto
- Bakuli / Beseni Kubwa
Namna Ya Kuzisafisha
- Unatakiwa kuchanganya apple cider vinega na maji yako ya moto katika bakuli au beseni lako, kama ukiweka kifuniko kimoja cha apple cider basi utatakiwa kuweka vikombe vitatu vya maji ya moto hakikisha unaweka maji ya kutosha ili rasta zako kuweza kulowekeka vyema.
- Kisha ziroweke kwa dakika kumi na tano (15), usitoe rubber band wala usijaribu kuzichana ziingize kwenye maji kama zilivyo ili usiziharibu ukashindwa kuzisukia, baada ya dakika kadhaa utaona vitu vyeupe juu ya maji vikielea, hio ndio kemikali inatoka.
- Baada ya dakika kumi na tano toa rasta zako na zikaushe kwa hewa ( airdry) usijali kuhusu harufu itaisha pale rasta zitakapo kauka vyema, lakini pia hakikisha zimekauka vyema kabla ya kuzisukia.
- Baada ya hapo unaweza kuzisukia kama kawaida.
Oyeeeee!!! Mambo ni moto mambo ni fireee mimi nimehitimisha wajibu wangu bwana kazi kwako mrembo mwenzangu kupambania urembo wako have a nice wikiend.
Leave a Reply