Mbappe nahodha mpya Ufaransa

Mbappe nahodha mpya Ufaransa

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St-Germain (PSG) Kylian Mbappe ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ufaransa ambapo mshambuliaji huyo anamrithi mlinda mlango wa Tottenham Hugo Lloris, ambaye alistaafu soka la kimataifa Januari mwaka huu.

Mbappe mwenye umri wa miaka 24, ameichezea Ufaransa michezo 66 tangu alipocheza mechi yake ya kwanza mnamo mwaka 2017.

Kupitia mahojiano yake na chombo cha habari nchini humo cha TF, kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps alieleza kuwa “Kylian amekidhi vigezo vyote vya kuwa na jukumu hili”

Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) lilithibitisha kuwa Deschamps amemteua Mbappe kama nahodha na mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann kama nahodha msaidizi.

Mbappe alikuwa mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana alipoisaidia Ufaransa kufika fainali ya pili mfululizo ya Kombe la Dunia, ambapo walifungwa na Argentina.

Alifunga mabao mawili kwenye fainali ya 2018 dhidi ya Croatia na alitajwa kuwa mchezaji bora chipukizi wa michuano hiyo huku Ufaransa wakitawazwa mabingwa wa dunia kwa mara ya pili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags