Mchezaji wa ‘klabu’ ya Paris Saint-Germain (PSG) Kylian Mbappe ametangaza kuondoka katika ‘timu’ hiyo ifikapo mwezi Julai baada ya mkataba wake kuisha.
Mbappe ametoa taarifa hiyo kwa Rais wa ‘klabu’ Al-Khelaifi, licha ya kutokukubaliwa kuondoka katika timu hiyo.
Endapo atafanikiwa kuondoka Mbappe ataondoka kama mchezaji huru huku tetesi zikidai kuwa yupo katika mazungumzo na Real Madrid toka Januari mwaka huu.

Leave a Reply