Mbappe alikubali sanamu lake asilimia 100

Mbappe alikubali sanamu lake asilimia 100

Nyota wa ‘timu’ ya Taifa ya Ufaransa ambaye anajiandaa kuondoka katika ‘klabu’ ya Paris Saint-Germain (PSG) Kylian Mbappe amelikubali sanamu lake lililozinduliwa siku ya jana Alhamis Mei 16 kwa asilimia 100.

Sanamu hilo mkali wa soka lilizinduliwa katika hafla ya ‘Madame Tussauds’ jijini, Paris ambapo mchezaji huyo alisikika akisema kuwa sanamu hilo limefanana na yeye kwa asilimia 100 “Huyu ni zaidi ya Kylian”.

Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la L'Equipe, lilieleza kuwa mtengenezeji wa sanamu hilo alichukua zaidi ya saa nne kutazama uso pamoja na mwili wa mchezaji huyo kutengeneza kitu kizuri.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags