Maua Sama: Naogopa sana magari

Maua Sama: Naogopa sana magari

Hahahahah! Make hapa kwanza nchike, wakati mimi na wewe msomaji tukitamani kumiliki mandinga na kutamba nayo mitaani kumbe kuna wenzetu wanayo ila hawawezi kuyatumia.

Basi bwana mwanadada Maua Sama amefunguka kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari alipoulizwa kuhusiana na kuwa na magari mangapi na huwa anaendesha mwenyewe au, alifunguka na kueleza kuwa…

“ Nimejaribu kuendesha nimeenda drive school lakini naogopa sana magari especially kukiwa kuna foreni kukiwa kuna watu wanavuka bila mpangilio, nimeanza kuwa na magari muda mrefu lakini siwezi kuendesha” amesema Maua Sama

Duh! Kama tunavyojua kila mja lazima awe na mambo yake private sasa yeye akitaka kwenda katika mambo yake ya siri inakuwaje, mwanadada huyo alifunguka…

“ Naendeshwa na Mark ni meneja, ikiwa naenda kwenye vitu private basi inakuwa private yetu wote lazima niende nae, siwezi kuendesha kabisa, sehemu yote inayo hitajika niende na gari lazima niendeshwe” amesema mwanadada huyo

Mmmmh! Haya mwanangu sana unayapi ya kutiririka hapo chini au kutiririka tumuachie dada Yammi, je unaweza kununua gari na usiendeshe?.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags