Mastaa na mitupio ya mavazi mwaka 2023

Mastaa na mitupio ya mavazi mwaka 2023

Leo katika Fashion tumekusogezea  baadhi ya wasanii waliotokelezea katika upande wa mavazi na wale ambao waliwashangaza watu kwa mitindo ya mavazi yaani walitoa booko hahahahaha!!!

 

WASANII WALIOPENDEZA  KIMAVAZI

*Wema Sepetu na vazi la abaya

Kwanza kabisa ukizungumzia swala la mitindo kwa msanii huyu hapa umefika ila huu mwaka asilimia kubwa alitokelezea katika mavazi yake hasa kwenye event mbalimbali lakini kuna vazi moja ambalo lilikuwa tofauti kwake ni Abaya ni vazi fulani lenye mahadhi ya heshima lakini kwa mwaka huu pia limekuwa kama vazi ka fashioni husani kwa hapa Bongo so vazi hilo lilimtoa sana.

 

*Hamisa Mobetto and fur coat (vazi la manyoya)

Likizungumzwa jina la mwanadada huyo wapo wanaosema linabeba maana halisi ya mitindo kwani maisha yake kwenye uvaaji hayana mbambamba hajawahi kutoka vibaya katika upande wa mavazi.

Lakini katika huu mwaka vazi ambalo lilikuwa bora zaidi na lipo katika fashion ni vazi la manyoya ambalo alivaa katika birthday yake lilimtoa sana, si hivyo tu aina hiyo ya vazi la manyoya aliweza kulirudia tena ndani ya mwaka huu ikiwa ni gauni ndefu iliyonakshiwa manyoya ya kutosha, kwa ufupi moja kati ya vazi lililomto na kuonekana wa tofauti.

*Irene Paul vazi la usiku wa tuzo

Irene au tunaweza kumuita ‘NaturalStar’ ni moja kati ya wasanii ambao tunaweza kusema ni wakamiaji wa event  huwa anatoka kitofauti sasa.  Katika usiku wa wa tuzo za ‘Film Festival’ yeye alivaa gauni alilobuni mwenyewe.

Kwanza lipo kwenye fashion lakini pia lilimtoa vizuri kwa ufupi alipendeza siku hiyo, hata hivyo watu wengi walionesha kupendezwa na vazi hilo lake kwa ufupi sisi watu wa fashion tunaweza kusema ni mmoja kati ya vazi bora na zuri ndani ya usiku huo wa tuzo.

*Vazi la Zaylissa usiku wa Tuzo za Film Festival

Pia muigizaji wa tamthilia pendwa ya ‘Jua kali’ Zaylissa au Maira alipendeza sana katika usiku huo wa tuzo kwa kuvaa vazi ambalo lilikuwa very simple na lenye utofauti alionekana vizuri katika usiku huo huku akipangilia aina ya mtindo kuanzia juu hadi chini.

*Fahyvanny na vazi la suti

Katika muonekano ambao alitokelezea mwaka huu mwanadada Fahyvanny ni vazi la suti ambalo alilivaa siku ambayo alipewa ubalozi katika kampuni ya biashara, hiyo siku alitoka smart na simple

*Gigy Money vazi la manyoya

Gigy money ni moja kati ya watu waliotokelezea mwaka huu katika upande wa mavazi  katika event mbalimbali amekuwa akifululiza kuvaa mavazi yaliyonakshiwa na manyoya.

 

WASANII WALIOHARIBU

 

*Yammi na vazi la manyoya

Yammi ni msanii ambaye anachipukia katika muziki wa Bongo fleva lakini kuna baadhi ya watu huwa wanamkosoa aina ya mavazi anayovaa

kuwa hayaendani kabisa na muonekano wake kwa ufupi kwenye uvaaji bado hajawakosha mashabiki.

Yammi mwaka huu alivaa vazi lenye rangi ya pink fur outfit ambayo ilikuwa  crop top, mini skirt na knee length fur socks zikiwa za manyoya ya pink, watu wengi walionekana kufananisha kivazi hiki na zulia la manyoya kwa ufupi hakuwa katika muonekano wa kuvutia.

*Kajala Frida na vazi la birthday

Mwaka huu kulizuka mambo mengi katika mtindo wa mavazi wa muigizaji Kajala, kuna wale waliosema mavazi hayaendani na umri wake, lakini vazi alilovaa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ilileta picha ya tofauti katika jamii.

Alivalia gauni ambalo lilikuwa la kuonesha sana mwili wake ambapo mashabiki wake hakuweza kulielewa ingawa lilikuwa zuri kimuonekano.

Licha ya hayo mwaka huu moja kati ya vazi lililo valiwa na wasanii katika event mbalimbali ni mavazi la manyoya limeonekana kupendwa sana na ‘mastaa’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags