Mashabiki wamnanga John Legend

Mashabiki wamnanga John Legend

Mashabiki wamemnanga mwanamuziki wa Marekani John Legend baada ya kuimba vibaya wimbo wa marehemu mwanamuziki Price katika mkutano wa Kitaifa wa Kidemokrasia (DNC).

Kupitia mitandao ya kijamii baadhi ya wadau wamemnanga na kumrushia maneno machafu msanii huyo wakidai kuwa show ilikuwa ni nzuri lakini hakupaswa kuuimba wimbo wa Prince kwani hakuutendea haki wimbo wa msanii huyo aliyefariki.

Naye aliyekuwa meneja wa msanii Prince, L. Londell McMillian alifunguka kwa kuweka wazi kuwa yeye hana tofauti na maoni ya mashabiki kuwa hakuutendea haki wimbo wa Prince uitwao ‘Let's Go Crazy’ licha ya kufanya kazi nzuri katika tamasha hilo.



Hata hivyo mashabiki walimwagia sifa mpiga gitaa wa muda mrefu wa Prince, Shelia E kwa kulinogesha tamasha huku wakimtaka Lenged kutorudia tena kufanya hivyo kwani atawafanya watu waache kufuatilia kazi zake.

Ikumbukwe kuwa Prince Rogers Nelson alizaliwa June 7, 1958 na kufariki April 21, 2016 akiwa na umri wa miaka 57 sababu ya kifo chake ikitajwa ni kuzidisha fentanyl, dawa ya opioid.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags