Mashabiki wahoji mabadiriko ya mdomo wa Kanye

Mashabiki wahoji mabadiriko ya mdomo wa Kanye

Baada ya kuweka Grill kwenye meno yake, mashabiki wameona tofauti katika lips za ‘rapa’ Kanye West huku wakihoji nini kimetokea mpaka muonekano wa mdomo wa mwanamuziki huyo kuwa tofauti.

Minong’ono hiyo inakuja baada ya kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii wakati ‘rapa’ huyo alipokuwa akieleza kuhusiana na haki aliyonayo ya kum-post mkewe Bianca Censori, ndipo mashabiki kuona mabadiliko ya mdomo wake.

Aidha kwa mujibu wa Page Six, imefanya mahojiano na Daktari maarufu kutoka New York, Clement Kairouz ambapo ameeleza kuwa ukuwaji wa lips hiyo unatokana na Grill alizoziweka, wakati wa kuongea Grill hizo husukuma mdomo wa juu.

Ikumbukwe kuwa Januari 17, mwaka huu Kanye West aliweka Grill katika meno yake zenye thamani ya dola 850K ambayo ni zaidi ya tsh 2.16 bilioni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags