Mashabiki wa Nigeria wafanya utani waimba Water ya Tyla

Mashabiki wa Nigeria wafanya utani waimba Water ya Tyla

Baada ya ‘timu’ ya taifa ya Nigeria kuifunga Afrika Kusini na kutinga katika Fainali za #AFCON mashabiki wa ‘Super Eagles’ wameonesha utani wao kwa kuimba wimbo wa mwanamuziki kutoka Afrika Kusini #Tyla wa ‘Water’.

Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya ‘penati’ ambapo Nigeria walishinda mabao 4-2 wakifuzu kuingia final ya #AFCON.

Mchezo mwingine uliochezwa jana ni kati ya Ivory Coast dhidi ya DRC Congo ambapo wenyeji Ivory Coast walitinga fainali baada ya kuichapa Congo bao 1-0.

Fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kucheza siku ya Jumapili Februari 11, huku ‘mechi’ ya mshindi watatu ikipigwa Jumamosi, Febriari 10.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post