Bodi ya maziwa nchini Kenya imepiga marufuku uagizaji wa maziwa ya unga kwa muda usiojulikana ili kuwalinda wasindikaji wa ndani na wakulima kutokana na uzalishaji wa ziada na bei ya chini kwa kutarajia mvua ndefu.
Msimu wa mvua unatarajiwa kuboresha uzalishaji wa malisho ya mifugo na kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa maziwa nchini, hivyo basi kupunguza hitaji la kuagiza kutoka nje.
Bodi hiyo ilisema itaendelea kufuatilia uzalishaji na mahitaji ya bidhaa hiyo kabla ya kuondoa marufuku hiyo na kusitisha utoaji wa vibali kutoka nje ya nchi.
Aidha hatua hiyo inaonekana kwenda kinyume na makubaliano ya biashara huria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu usafirishaji huria wa bidhaa na huduma na soko la pamoja.
Uganda na Rwanda ndizo nchi zinazoongoza barani Afrika kwa uzalishaji maziwa.
Leave a Reply