Marufuku saloon za kike, Afghanistan

Marufuku saloon za kike, Afghanistan

Kundi la Taliban limeamuru saluni za nywele na urembo za kike nchini Afghanistan kufungwa ikiwa ni kikwazo kipya wanachokabiliana nacho wanawake.

Taliban imewapa wanawake wa Afghanistan mwezi mmoja kutekeleza agizo hilo, kuanzia tarehe 2 Julai walipofahamishwa kwa mara ya kwanza kuhusu hatua hiyo.



Uhuru wa wanawake umepungua kwa kasi tangu Taliban kuchukua mamlaka 2021. Huku wakiwazuia wasichana na wanawake kuhudhuria madarasani, kumbi za mazoezi na hata katika bustani, na hivi karibuni zaidi waliwapiga marufuku kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags