Marubani wa Kenya Airways kuanza mgomo kesho

Marubani wa Kenya Airways kuanza mgomo kesho

Marubani wa shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, wataanza mgomo kesho kutilia mkazo madai yao ya mazingira bora ya kazi, licha ya mahakama ya nchi hiyo kuamuru mgomo huo usitishwe.

Kenya Airways inayomilikiwa na serikali ya Kenya na shirika la ndege la Uholanzi, KLM, ni mojawapo ya mashirika makubwa ya usafiri wa anga barani Afrika, ikiunganisha miji mingi katika mabara ya Afrika, Asia na Ulaya.

Katibu Mkuu wa chama cha marubani wa Kenya Airlines, Kapteni Murithi Nyaga, amesema hakuna ndege ya shirika hilo itakayopaa kutoka uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi kuanzia saa 12 asubuhi kesho Jumamosi, akisema uongozi wa shirika hilo umeshindwa kushughulikia malalamiko ya marubani.

Kenya Airways ilionya siku ya Jumatano kwamba malalamiko ya marubani hao hayana uzito wa kuhalalisha mgomo.

Chanzo DW

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags