Martin Lawrence afichua sababu ya kukataa kuigiza na Jackie Chan

Martin Lawrence afichua sababu ya kukataa kuigiza na Jackie Chan

Mwigizaji kutoka Marekani Martin Lawrence amefichua siri kuwa aliwahi kuombwa kuigiza pamoja na mkali wa filamu za mkono Jackie Chan katika filamu ya ‘Rush Hour’ ya mwaka 1998 lakini alikataa kushiriki katika filamu hiyo.

Wakati akiwa kwenye mahojiano yake na Will Smith katika kipindi cha ‘The Tonight Show’ Lawrence alieleza kuwa alikutana na Chan kwa chakula cha jioni na walizungumza kwa muda mrefu lakini hawakuweza kufikia muafaka kutokana na maokoto kuwa madogo.

Aidha baada ya filamu hiyo kupata mafanikio na mapato zaidi wadau mbalimbali walianza kumshambulia Lawrence kutokana na kukataa ofa hiyo, lakini kwa upande wake amedai kuwa alifurahi sana kuona ‘Rush Hour’ imepata mafanikio kwa kiasi kikubwa huku akikubali zaidi uigizaji wa Chris Tucker na Jackie Chan.

Kwa sasa Martin Lawrence na Will Smith wanatarajia kuonesha filamu yao ya‘Bad Boys 4’ itakayoanza kuoneshwa katika kumbi za sinema Juni 7, 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags