Katika usiku wa ugawaji wa Tuzo za Grammy mwaka 1984 marehemu mkali wa Pop Marekani, Michael Jackson aliwashangaza wengi baada ya kuvua miwani yake mbele ya umati wa watu.
Kama ijulikanavyo kuwa msanii huyo alikuwa si mwepesi wa kuvua miwani yake mara kwa mara, wakati alipokwenda kupokea tuzo yake ya Best Pop Vocal Performance, Male alivua miwani aliyovaa jambo ambalo lilisababisha shangwe kwa wahudhuriaji katika tuzo hizo.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali MJ aliweka wazi kuwa aliamua kuvua miwani hiyo kama ishara ya kutimiza ahadi ya rafiki yake mwigizaji Katharine Hepburn ambaye alimuahidi kufanya hivyo baada ya kuondoka na tuzo hiyo.
Usiku huo MJ alishinda Tuzo nane za GRAMMY huku akijiwekea rekodi ya pekee ambapo aliondoka na tuzo kama Album of the Year na Best Pop Vocal Performance – Male (Thriller); Record of the Year na Best Rock Vocal Performance – Male (Beat It); Best R&B Song na Best R&B Vocal Performance – Male (Billie Jean); Producer of the Year – Non-Classical na Best Recording for Children (The E.T. Storybook).
Michael Jackson, maarufu kama "Mfalme wa Pop," alizaliwa Agosti 29, 1958, huko Gary, Indiana, Marekani na kufariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 50.
Leave a Reply