Manara: Tunataka ‘marefa’ watenda haki

Manara: Tunataka ‘marefa’ watenda haki

"Kesho ni ‘mechi’ ya hisia kubwa ni mechi yenye kuchukua akili za watanzania, sio ‘mechi’ ya matokeo tu bali ni ‘mechi’ inayosakwa heshma zaidi miongoni mwetu,wachezaji, ‘makocha’, viongozi na hasa mashabiki.

Tunajua raha ya wakubwa ni kuona derby pale Tanga lakini aina hii ya waamuzi hatutaki kuwaona, msituletee waamuzi wa aina hii, mwamuzi aliyetoka nyumbani kuja kufunga kibwebwe cha mbeleko ni marufuku kesho.

Referees wa kesho wawe Watu wanaotoka makwao kuja kutenda haki, asipendelewe mtu na asionewe yeyote, Bingwa halali apatikane uwanjani sio kwenye korido na viwambaza vya Tanga!!"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags