Manara: Kwangu wamebugi

Manara: Kwangu wamebugi

Uwiiiiiiii! Hahahha! Make hapa kwanza ncheke,  Semaji la mabingwa bwana hajaamua kukaa kimya baada ya sakata lake kufungiwa na TFF miaka 2 na faini ya million 20 Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameendelea kuwakera Zaidi na kuwaambia kuwa hapoi hata kidogo labda waje kumuua.

Manara amefunguka huku akiwa ameshare video ya siku ya wananchi mwaka jana  na kueleza kuwa “kumbe tatizo ni hili? Uhhh lalalaah!!, wamebugi kwangu sitawaacha wananchi na litakuwa tamasha kubwa kuliko walivyo fikiria” aliendelea kwa kuandika

“kwa Watu wa football na Sports kwa ujumla kunizidi ,,nguvu hiyo niliojaaliwa na Mungu,nitaitumia effectively kulipush hili Concert kuu la kisoka, Ikiwa Parade yetu ilivunja Rekodi why tushindwe hili?
Msifadhaike hata kidogo, tuombe uhai tu coz dhulma huwa haina mwisho mwema na always haki hushinda, ni suala la muda tu” amesema Manara

Aidha aliendelea kwa kuongezea kuwa “Sipoi hata tone na tabu ipo pale pale, sana sana ndio itazidi otherwise waje kuniua,Yanga Bingwa na mimi ndio Bugati


Byuti Byuti

Alooooooo! Kama nawaona wananchi, kama wewe ni mwanachi dondosha komenti yako hapo chini.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags