Man United yaitajia Dortmund bei ya Sancho

Man United yaitajia Dortmund bei ya Sancho

‘Klabu’ ya Manchester United inataka walau asilimia 75 ya kiasi cha pesa ilicholipa kumnunua Jadon Sancho mwaka 2021 ikiwa ‘timu’ yoyote itataka kumsajili mwisho wa msimu huu.

Sancho ambaye alinunuliwa kwa Pauni 75 milioni anadaiwa kuwa katika rada za Borussia Dortmund inayotaka kumsainisha mkataba wa kudumu baada ya ule wa mkopo kumalizika.

Hata hivyo, ili kukamilisha uhamisho wa kutua Dortmund atatakiwa kukubali kupunguza mshahara wa Pauni 275,000 kwa wiki anaoupokea.

‘Timu’ nyingi zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Sancho kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu akiwa na Dortmund hadi kuisaidia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa ripoti ‘kocha’ wa Mashetani Wekundu, Erik Ten Hag hana mpango wa kumtumia staa huyo kwa msimu ujao na amekubali auzwe.

Tangu atue Dortmund, Januari, mwaka huu amecheza mechi 20 za michuano yote, amefunga mabao matatu na ametoa asisti tatu kikiwa ni kiwango bora zaidi kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags