Man United mbioni kumtangaza mkurugenzi mpya

Man United mbioni kumtangaza mkurugenzi mpya

Klabu ya #ManchesterUnited inajiandaa kusaini nyaraka kwa ajili ya kumtangaza Dan Ashworth kama Mkurugenzi wa Michezo kutoka klabu ya Newcastle United baada ya vilabu hivyo kuafikiana juu ya fidia.

Inaelezwa kuwa Ashworth mwenye umri wa miaka 53 raia wa England amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa West Bromwich Albion na Brighton na Hove Albion pamoja na kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la kulipwa wa chama cha soka England (FA).

Touti ya Sky Sport News imeeleza kuwa Ashworth atatangazwa na kuanza kazi katika klabu hiyo kama mkurugenzi Julai 13 mwaka huu.

Ashworth akiwa Brighton na Newcastle, mkurugenzi huyo alifanikisha usajili wa baadhi ya nyota  wa soka kama Moises Caicedo, Alexander Isak, Alexis Mac Allister, Leandro Trossard, Evan Ferguson, Nick Pope, Kaoru Mitoma, Marc Cucurella, Anthony Gordon na Sven Botman.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags