Mambo magumu kwa Diddy ashindwa kuhudhuria mahafali ya binti yake

Mambo magumu kwa Diddy ashindwa kuhudhuria mahafali ya binti yake

Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy ameripotiwa kuwa hatokuwepo kwenye mahafari ya binti yake itwaye Chance (17) huku wadau wakieleza kuwa hatohudhuria katika sherehe hiyo kufuatia na kesi zinazo mkabili.

Kwa mujibu wa Tmz mahafari ya #ChanceCombs yatakayofanyika katika Shule ya Sierra Canyon huko Los Angeles yatahudhuriwa na familia ya Kim Porter pamoja na mama mzazi wa Chance, Sarah Chapman.

Hii inakuwa mara ya pili kwa #Diddy kutohudhuria kwenye matukio makubwa ya watoto wake kwani wiki iliyopita alishindwa kuhudhuria kwenye shughuli ya tangazo la biashara ya watoto wake mapacha #Jessie na D'Lila.

#Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa ngono toka mwishoni mwa mwaka jana, ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana na kesi hizo mahakamani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags