Mama mzazi wa Costa Titch adai vipimo vya maabara

Mama mzazi wa Costa Titch adai vipimo vya maabara

Mama mzazi wa marehemu Costa Titch aitupia lawama maabara ya kitaifa ya afya kwa kuchelewesha kutoa majibu ya vipimo kuhusu kifo cha mtoto wake akidai kwamba aliwekewa sumu.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mwanae ameandika kuwa “Maabara ya kitaifa ya afya, huduma inaweza kuchukua miezi au hata mwaka kukamilisha vipimo vya sumu. hii inamaanisha kuwa mimi sio mama pekee Afrika Kusini ninayetakiwa kusubiri majibu”

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa “inamaanisha kama kuna mtu alihusika kumpa mwanangu sumu anaweza kuondokana na mauaji, naomba msaada wa majibu kwani hata polisi hawawezi kufanya lolote bila majibu ya vipimo kutoka maabara” ameandika mama mzazi wa marehemu Costa Titch

Ikumbuka rapa huyo alifariki dunia machi 12 mwaka huu akitumbuiza jukwaani huko mjini johannesburg, South Africa.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post