MAKUYA DOMINIC: Tutumie bando za simu kujifunza vitu mtandaoni

MAKUYA DOMINIC: Tutumie bando za simu kujifunza vitu mtandaoni

Makuya Dominic ni kijana mcheshi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwenye ndoto za kumiliki shule yake na kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kuuza kompyuta, simu, nguo na viatu.

Hata hivyo Dominic aliyewchukua kozi ya Bachelor of Art With Education (Geography na Linguistics) ameanza haraka za kufanya biashara muda mrefu na anatamani ndoto hiyo iweze kufanikiwa.

Akizungumza na mwananchiscoop, anasema licha ya kutamani kuwa mfanyabishara anataka vijana kuhakikisha wanatumia bando za simu kujifunza vitu mitandaoni hasa za kuwaingizia kipato.

Anasema vijana wengi wamejisahau na kujikuta wakitumia simu kuangalia umbea na mambo yasiyofaha na kusahau kuwa wanaweza kuitumia kwa kuangalia fursa mbalimbali za kufanya biashara.

“Bando wanazoweka kwenye simu vijana wenzangu tuzitumie kujifunza vitu vingi mitandaoni ambavyo vitatufanya tusiwe tegemezi na si kutumia kwa kujiburudisha, pia tujitahidi kushiriki matukio mengi kama semina na mikutano ambayo itatuongezea ujuzi na maarifa,” anasema

Mwanakaka huyu ambaye pia anapenda kuja kuwa mwanasiasa na mwigizaji wa filamu mbalimbali ikiwemo za uchekeshaji zenye lengo la kuelimisha jamii.

Anasema kwa sasa anafanya biashara ya uwakala wa kuuza kompyuta, kutengeneza kompyuta na simu za mkononi kwa mfumo ya software, kuandaa matangazo na kufanya video editing anasema anajivunia kufanya mambo hayo.

Anasema aliamua kujikita kwenye hizo biashara kwa kuwa aliwaza kwamba dunia ya sasa vitu vingi wanavyofanya vinahitaji teknologia.

“Hivyo nilianza kutumia muda wangu wa ziada kusoma kwa njia ya mtandao namna ya kushugulika na kompyuta, simu video editing na kuandaa matangazo, nikaanza kufanya mazoezi kwa wingi na mwisho wa siku nikawa vizuri kwenye hizi fani na nikaanza kupata pesa kupitia hizo, nilikuwa natumia sana maktaba ya chuo kwa sababu kuna internet ya bure kwa wanafunzi,” anasema.

Changamoto

Anasema moja ya changamoto anazokutana nazo ni kukutana na matatizo mageni ambayo hajawahi kutatua hasa kwenye kompyuta na simu.

“Lakini yananifanya kuumiza kichwa kutafuta suruhisho ili ijapo tena tatizo kama hilo nisipate shida. Kwenye uwakala wa kuuza kompyuta, changamoto kubwa ni wateja kugaili kufanya biashara, mfano mtu anaweza kukuagiza nahitaji kompyuta au kifaa cha kompyuta, nahangaika kumtafutia dukani na mwisho wa siku anaghaili.

“Cha mwisho katika computer software repairing, nakutana na changamoto za viruses zinashambulia baazi ya devises lakini maisha yanaendelea,” anasema

Hata hivyo anasema biashara hizo anazozifanya ndizo ambazo zinampatia uhakika wa kuishi chuoni.

“Nilikuwa na mkopo lakini asilimia 99 nilikuwa naitoa kusaidia familia, hivyo biashara hizi zinanifanya nipate fedha za kujikimu.  Lakini pia shughuli hizi zimenifanya kuwa mtu mwenye ujuzi mwingi.

“Natumaini hata baada ya chuo naendelea kuzifanya. Ingawa bado sina ofisi  maalumu kwa sababu mara nyingi nawafata wateja walipo, nina mpango wa kuwa na ofisi yangu kubwa ambayo itajikita kuuza na kutengeneza  kompyuta na simu kwa mfumo wa software na hata hardware kwa sababu nipo kwenye mchakato wa kujifunza hardware repairing,” anasema.

Ushauri wake

“Ushauri wangu kwa vijana ni kwamba wasiishi kwa kutegemea fani moja, wawe wabunifu wa kufanya vitu vingi. Wawapo chuoni watumie rasilimali za vyuo kupata juzi nyingi zaidi ya wanazosomea, hasa kwa kutumia maktaba za vyuo, hasahasa kompyuta wanaweza kujifunza fani nyingi mitandaoni.

Aidha anasema anapenda kufundisha kwa sababu ndo fani ambayo pia amesomea chuoni.

“Ninawazo la kuwa na shule yangu. Pia napenda kufanya biashara ya nguo na viatu, pia nina kalama ya uongozi, napenda siasa. Napenda pia sanaa ya uigizaji. Nina channel yangu inaitwa Mr Makwazo Instagram na YouTube. Napenda kuimba gospel music,” anasema na kuongeza

“Kwanza napenda toka moyoni, nafurahia kuwa hivyo. Nakuwa na amani kuwa katika hizo Nyanja.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags