Makosa ya wanawake katika kuchagua wenza

Makosa ya wanawake katika kuchagua wenza

Ngoja leo niyadadavue makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua ni nani wa kuoana naye:

1. Kosa la kwanza, unaolewa na mtu ambaye unajua kabisa ni dhaifu na mkorofi, ukitarajia kwamba ataondoa kasoro zake akiwa ndani ya ndoa. Hili ni kosa kubwa. Kama huna furaha sasa na mtu kabla hujaoana naye, usikubali kuingia huo mkenge. Huwezi kutegemea mtu kuadilika aiwa ndani ya ndoa.

2. Kosa la pili, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu ya msisimko wa mwili kimapenzi lakini si kwa sababu ya tabia zake. Kuwa mwangalifu na neno “Nakupenda” neno hili mara nyingi maana yake ni “Nina uchu nawe.” Ndiyo amevutiwa nawe kimaumbile, lakini undani wa tabia yake unaujua? Hapa kuna mambo manne… Kwanza, Je anapenda kutomfanyia binadamu mwenzie mabaya kama ambavyo yeye hataki kufanyiwa? Pili, anaishi vipi na watu wengine? Anaishi vipi na watu ambao ana uadui nao, Anawasamehe au analipiza visasi? Je anatoa misaada kwa masikini? Tatu, je ni mkweli, anachokisema ndicho anachokifanya? Je anaaminika? Majukumu anayoahidi kuyafanya anayatimiza? Nne, je anajipenda? Je ni mtu ambaye yuko imara kimapenzi au ni mtu wa kuyumbayumba na asiye na msimamo? Sio mtu akishauriwa na marafiki zake au ndugu zake huko, anakuja na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu

3. Kosa la tatu, unaolewa na mtu ambaye hamna malengo na vipaumbele vya aina moja vya maisha. Je mna utashi wa aina moja? Kwa mfano ni vyema mwanamuziki akaolewa na mwanamuziki mwenzie kwa kuwa anajua mzingira ya kazi ya mwenzie ili kupunguza wivu wa kupindukia usio wa lazima

4. Kosa la nne, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu mnakutana kimwili mapema mno. Kukutana kimwili kabla ya ndoa kunaweza kuleta matatizo makubwa mno. Tendo la ndoa kabla ya ndoa hufunika uwezo wa mtu kufikiri. Mtu anabaki kufaidi na kubaki kujali mapenzi ya kimwili na kusahau kukuna ubongo juu ya mambo mengine. Ni lazima mwanamke akune ubongo ili kujua kama huyo mpenzi anakidhi vigezo vyote vya mume mtarajiwa.

5. Kosa la tano, unaolewa na mtu ambaye huna msisimko wa kimwili umwonapo. Kuna uwezekano mkubwa mwanamke akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya aina ya gari analomiliki. Hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutwa na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo.

6. Kosa la sita, unaolewa na mwanaume anayependa kudhibiti. kuwa na tabia ya kudhibiti wenzako ni ya dalili za mtu jeuri na mwenye kujisikia na mfujaji. Naomba kutofautisha kati ya “kudhibiti” na “kutoa mawazo.” Mtu anayekupa mawazo ni kwa faida yako, lakini anayekudhibiti ni kwa faida yake.

7. Kosa la saba, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu unakimbia matatizo uliyo nayo. Unaweza kuwa hujaolewa na huna raha wala amani na ukataka kuolewa. Ndo haiwezi kukutatulia matatizo yako binafsi ya kisaikolojia na ya kimapenzi. Badala a kuyapunguza matatizo hayo, ndoa itayaongeza. Kama huna amani na huyafurahii maisha, chukua jukumu la kurekebisha matatizo hayo sasa kabla hujaolewa. Itakuwa ni faida kwako na kwa mumeo mtarajiwa.

8. Kosa la nane, unaolewa na mtu asiya sahihi kwa kuwa yuko ndani ya pembe tatu. Mtu ambaye anaishi na wazazi wake ni moja ya mfano wa mtu anayeishi katika pembe tatu. Watu wengine wanaoweza wakawa wanaishi ndani ya pembe tatu ni kama wanaofanya kazi saa 24! Huyu mtu halali? Watu wengine walio katika pembe tatu ni watu wanaotumia madawa ya kulevya, mtu anayetawaliwa na “hobbie” zake, anapenda sana michezo (Mpira), kuperuzi mitandao ya kijamii na anapenda sana fedha. Hakikisha kwamba wewe na mpenzi wako , nyote hamtawaliwi na pembe tatu. Mtu ambaye anatawaliwa na pembe tatu hawezi kumtimizia mpenzi wake haja ya upendo atakapokuwa anahitaji. Kama mpenzi wako anatawaliwa na pembe tatu kwa kiasi kikubwa, wewe huwezi kuwa kipaumbele chake.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post

Latest Tags