Lulu: Simlaumu mama Kanumba

Lulu: Simlaumu mama Kanumba

Baada ya muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) kuonekana kwenye video akiwa anasalimiana na mama yake marehemu Kanumba, na video hiyo kuonesha kuwafurahisha wafuasi wengi wa mitandao ya kijamii sasa Lulu atoa neno kuhusiana tukio hilo.

Lulu amedai kuwa anafurahia, na anashukuru Mungu kwani vitu vilivyotokea ni vya kibinadamu hivyo basi hamlaumu mama Kanumba kwa chochote kilichotokea kwani ni mzazi anauchungu hivyo ni haki yake kufanya chochote.

Hata hivyo Lulu amesema anafurahi sasa kwani mama huyo kwa sasa anafuraha. Ikumbukwe siku za nyuma tangu kufariki kwa muigizaji Kanumba mama huyo alikuwa akiumia na wakati mwingine kujikuta akitoa baadhi ya maneno dhidi ya Lulu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags