Lady Jaydee Amwaga Wino Universal Music East Africa

Lady Jaydee Amwaga Wino Universal Music East Africa

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Lady Jaydee ‘Jide’ ameendelea kuvuka mipaka sasa amesaini mkataba na lebo ya Kimataifa ya muziki ya ‘Universal Music East Africa’.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa kampuni hiyo umeweka wazi taarifa hiyo kwa kueleza kuwa moja ya jambo lililowafanya kuungana na msanii huyo ni kutokana na sauti, safari yake ya muziki na nyimbo zake zinazoibua hisia kwa mashabiki.

“Mwanamuziki mashuhuri wa Tanzania @jidejaydee amesaini mkataba na Universal Music, hatua muhimu sana katika safari yake ya muziki na tasnia ya muziki nchini. Akijulikana kwa sauti yake inayoibua hisia za mashabiki na nyimbo zake zilizoshika chati, Lady Jaydee amekuwa mstari wa mbele katika muziki wa Afrika Mashariki kwa zaidi ya miongo miwili (miaka 20).

“Ushirikiano huu na Universal Music, moja ya lebo kubwa zaidi za muziki duniani, unamweka Lady Jaydee kwenye nafasi ya kupenya kimataifa. Hatua hii inaonyesha ongezeko la shauku ya muziki wa Kiafrika kwenda Kimataifa hasa sauti za Kitanzania kama Bongo Flava. Pia inampa fursa ya kupata rasilimali za hali ya juu za uzalishaji, usambazaji, na masoko, jambo linaloimarisha uwezo wake wa kushindana kwenye jukwaa la kimataifa” imeandika taarifa hiyo

Hii sio lebo ya kwanza Jide kusaini utakumbuka kuwa miaka ya nyuma alisaini na lebo kama Rockstar, Taurus Musik ya Kenya na nyinginezo.

Mkongwe huyo katika muziki wa Bongo Fleva amewahi kutamba na ngoma zake kama Yahaya, Siku Hazigandi, Mambo matano, Ndi Ndi Ndi, Joto Hasira na nyinginezo nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags