Lady Gaga awaanika waliosema hatokuwa maarufu

Lady Gaga awaanika waliosema hatokuwa maarufu

Mwanamuziki na mwigizaji kutoka Marekani, Lady Gaga amelianika hadharani kundi la zamani la Facebook la chuo kikuu cha New York na kudai kuwa kundi hilo lilimwambia hatokuja kuwa maarufu kamwe.

Kundi hilo lililotambulika kwa jina la ‘Stefani Germanotta’ lilijitokeza wakati Gaga alipokuwa akifanya maonesho kwenye baa ndogo jijini Manhattan huku washiriki wa kundi hilo wakimdharau na kumdhihaki kwa maneno kuwa hatukuja kuwa maarufu.

Akisimulia kuhusu kundi hilo kupitia akaunti yake ya TikTok huku aki-share picha ya kundi hilo aliwashauri watu kutokukata tamaa, bali unachotakiwa kukifanya ni kuendelea mbele.

“Hii ndiyo sababu huwezi kukata tamaa pale watu wanapokudharau au kukukatisha tamaa, lazima uendelee mbele.” Alisema Gaga



Lady Gaga katika maisha yake kwenye tasnia ya muziki amefanikiwa kutoa ngoma kama ‘Bloody Mary’, ‘Bad Romance’, ‘Always Remember Us This Way’, ‘Poker Face’ huku album yake ya kwanza iitwayo ‘The Fame’ ikipenya Kimataifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags