Kuondoka kwa Klopp, Benitez adai kuna kitu

Kuondoka kwa Klopp, Benitez adai kuna kitu

‘Kocha’ wa zamani wa ‘klabu’ ya #Liverpool, #Rafa Benitez amedai kuwa kuna kitu nyuma ya uamuzi wa ‘kocha’ Jurgen Klopp kuondoka kwenye ‘timu’ hiyo mwisho wa msimu huu.

#Klopp alishtua wapenda soka wengi wiki iliyopita baada ya kuweka wazi mpango wake wakuondoka #Liverpool baada ya kutumikia ‘timu’ hiyo kwa misimu tisa.

‘Kocha’ huyo ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 56 alisema anaondoka kwa sababu amekosa tena nguvu ya kuendelea kuifundisha Liverpool kutokanana na ‘timu’ hiyo kuhitaji mabadiliko.

Hata hivyo Benitez ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Liverpool miaka hiyo amefunguka na kudai kuwa uamuzi wa #Klopp haukumshitua.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags