Kunguni waibukia Korea Kusini

Kunguni waibukia Korea Kusini

Ni wiki kadhaa zimepita tangu wadudu aina ya Kunguni kutawala jiji Paris nchini Ufaransa, wadudu hao wamegeuza muelekeo na kuibukia nchini Korea Kusini.

Kwa mujibu wa BBC imeeleza kuwa uvamizi huo wa kunguni nchini Korea Kusini uliripotiwa Septemba, katika chuo kikuu katika jiji la Daegu na baadaye waliripotiwa katika makao ya watalii, usafiri wa umma na kumbi za sinema.

Takribani matukio 17, kuhusu kunguni yameripotiwa, katika Mji Mkuu wa Seoul pamoja na Miji ya Busan na Incheon ambapo imedaiwa kuwa Seoul imetenga zaidi ya Dola laki tqatu kukabiliana na wadudu hao.

Huku wakazi wa eneo la Seoul wanadaiwa kumiminika katika vituo vya afya vya umma, wakitaka kuchunguzwa afya zao na kutafuta ushauri juu ya hatua wanazopaswa kuchukua.

Serikali ya Metropolitan ya Seoul imepanga kukagua baadhi ya vituo vya umma 3,200, pamoja na hoteli na mabafu, ili kutathmini hali zao za usafi.
.
.
.
#MwananchioScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags