Kundi la P-square lasambaratika kwa mara nyingine

Kundi la P-square lasambaratika kwa mara nyingine

Mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ amethibitisha kuwa kundi la P-Square limegawanyiuka kwa mara nyingine.

Tudeboy amelithibitisha kusambalatika kwa kundi hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na mapacha wawili ambao ni Peter Okoye na Paul Okoye akiwa kwenye mahojiano yake na ‘City FM’, ambapo alidai kuwa kundi hilo halipo tena kwani toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

“Hapana, P-Square haipo tena, hapo awali, sikusema chochote kuhusu hilo, kwa sasa ninazingatia tu Rudeboy, sijawahi kuzungumza, lakini kuna kitu kimenifanya nifunguke, hasa kipengele muhimu ambacho kinaendelea kuleta tatizo hili.

Kitu pekee muhimu kinacholeta matatizo haya, machoni pa umma, ni kuwa tuliporudi, hakukuwa hatukupiga hata picha ya pamoja, Hakuna meneja, hakuna mkurugenzi, hakuna chochote ni kama nilikuwa peke yangu” amesema Rudeboy

Hata hivyo mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 42 alifichua kuwa matatizo yao yalianza mwaka 2014 walipotoa wimbo wa ‘Ejeajo’ wakimshirikisha ‘rapa’ wa Marekani T.I ambapo walitengana kutokana na maoni potofu kwa umma kuhusu nani alimfunika mwenzie kwenye ngoma hiyo.

Utakumbuka kuwa kundi la P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka jana kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamegawanyika tena.

Wawili hao walitamba na ngoma zao kama ‘Taste The Money (Testimony )’, ‘Personally’, ‘Forever’ pia wamewahi kutoa ‘kolabo’ na mwanamuziki Diamond wimbo uitwao ‘Kidogo’






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post