Kukuruku asimulia Ruger alivyomwokoa

Kukuruku asimulia Ruger alivyomwokoa

Mtayarishaji wa muziki kutoka nchini Nigeria, #KukurukuBeats amefunguka na kutoa heshima kwa msanii #Ruger akidai kuwa amemfanya nyota yake ing’ae baada ya msoto wa muda mrefu bila mafanikio.

Kukuruku ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika kuwa, “Baada ya miaka 10 ya uzalisahaji na matokeo madogo nilijikatia tamaa hadi kufikia hatua ya kupata wazimu lakini Ruger alikuja kuniokoa.”

Aidha, mtayarishaji huyo amedai kuwa Ruger alimbeba kila ziara aliyokuwa anakwenda na kumlipia gharama zote za safari, hiyo ilimsaidia kujulikana kwa ukubwa zaidi.

Hata hivyo Kukuruku amekiri kuwa, kuna muda anapitia wakati mgumu kwa Ruge lakini ameapa kumpenda mpaka kufa na kumshukuru huku akimwita ndiyo Rais wake.

Kukuruku ametengeneza  nyimbo mbalimbali za wasanii nchini humo  akiwemo Chidinma, Solid Star, Rugged Man, Victor AD, na Ruger, pia amefanya kazi na wasanii kadhaa kutoka Marekani na sehemu zingine za ulimwenguni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags