Komasava yaendelea kumng’arisha Diamond

Komasava yaendelea kumng’arisha Diamond

Baada ya mwanamuziki Diamond kutamba zaidi na ‘Komasava Remix’ aliyomshirikisha msanii wa Marekani Jason Derulo, na sasa ametajwa kuwepo kwenye album ya ‘rapa’ Keenon Dequan Ray ‘YG’.

Album hiyo iliyopewa jina la ‘Street Love’ inatarajiwa kutoka hivi karibuni huku ikiwa na wasanii wakubwa waliyoshirikishwa akiwemo Ty Dolla sign, Saweetie na wengineo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Diamond ame-share listi ya nyimbo zilizopo kwenye album hiyo huku akiachia na ujumbe usemao ‘Yeah, Another problem is Coming’ akiwa na maana kuwa kuna shida nyingine inakuja.



Hata hivyo ‘rapa’ YG ametangaza kuwa album hiyo inatarajiwa kuachiwa rasmi Ijumaa hii Agosti 16, 2024.

Aidha baadhi ya wadau mbalimbali wametoa maoni mbalimbali kwa kueleza kuwa Diamond huenda akawa na msululu wa kufanya ‘kolabo’ na wasanii wa nje kutokana na wimbo wake wa ‘Komasava’ wenye zaidi ya watazamaji milioni 9.7 kwenye mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags