Kizz Daniel akanusha kukamatwa Ivory Coast

Kizz Daniel akanusha kukamatwa Ivory Coast

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Kizz Daniel akanusha taarifa ya yeye kukamatwa nchini Ivory Coast kwa madai ya kuwa alikataa kutumbuiza kwenye show moja nchini humo, licha ya kulipwa kiasi cha dola 150,000.

Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi, Oktoba 12, 2023, wakati Kizz Daniel kukataa kupanda jukwaani licha ya kufika eneo la tukio kutokana na hali hiyo,msanii huyo alikamatwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na kupelekwa kizuizini.

Lakini kupitia ukurasa wa Instagram wa msanii huyo amekanusha madai hayo kwa kueleza kuwa alifika na kutumbuiza kwa dakika 3 kwa sababu hakuna malipo yoyote aliyoyapokea hivyo basi amewaondoa hofu mashabiki wake kuwa hajakamatwa na CAF na yuko sawa kwa sasa anaelekea London kwa ajili ya show itakayofanyia Novemba 12.

Hii si mara ya kwanza kwa Kizz Daniel kukumbana na matukio kama haya ikumbukwe Agosti 2022 alikamatwa nchini Tanzania baada ya kutotokea katika show kwa madai ya kupotelewa na vitu vyake






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags