Kizz Daniel adaiwa kuachana na mkewe

Kizz Daniel adaiwa kuachana na mkewe

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Kizz Daniel ameripotiwa kuachana na mkewe, hii ni baada ya kufuta picha zote akiwa na mama watoto wake huyo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Kizz Daniel amefuta picha pamoja na video akiwa na mkewe aitwaye Mjay Anidugbe huku akibakisha posti chache za matangazo ya show zake ambapo kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo zinadai kuwa huenda wawili hao wakawa wameachana.

Hata hivyo kupitia ukurasa wa Instagram wa Mjay Anidugbe umeoneka kuwa active muda wote huku picha na video akiwa na mumewe Kizz Daniel zikiwa hazijafutwa.

Machi mwaka huu Kizz Daniel alithibitisha kufunga ndoa na mwanadada huyo toka mwaka 2020 na kudai kuwa hawezi kumuacha mke wake kutokana na anavyomvumilia kwa tabia zake mbaya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags