Kiungo wa Chelsea akosa mechi kisa upasuaji

Kiungo wa Chelsea akosa mechi kisa upasuaji

Kiungo wa klabu ya #Chelsea, #EnzoFernandez atakosa mechi zote zilizobakia za msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja ili awe ‘fiti’ kwa ajili ya kuichezea timu ya Argentina katika michuano ya Copa America.

Kwa mujibu wa The Sun News imeeleza kuwa upasuaji huo utamuweka nje wiki tatu na atakuwa tayari kucheza michuano ya Copa America inayoanza Juni 20, mwaka huu nchini Marekani.

Uamuzi huo wa kumfanyiwa upasuaji umetolewa baada ya madaktari wa timu hiyo kushauriana na madaktari wa timu ya Argentina kumfanyia upasuaji kiungo huyo.

Kuondoka kwa Enzo katika kikosi hicho inaweza kuathiri zaidi ubora wa timu kwenye mechi zilizobakia za kumalizia msimu ingawa walianza kuwa na hali mbaya tangu mwanzo wa msimu.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kufanyiwa upasuaji Fernandez alionekana kupinga suala hilo licha ya madaktari wa Chelsea na wa Argentina kutaka afanyiwe, aliamua kuwasiliana na daktari wake aliyekuwa anamtibia mara kwa mara tangu alipokuwa katika klabu ya River Plate ambaye pia alimwambia kwa tatizo lake upasuaji ni lazima.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags