Kisa usaliti Neymar na mpenzi wake waachana

Kisa usaliti Neymar na mpenzi wake waachana

Mwanasoka kutoka nchini #Brazil, #NeymarJr na mpenzi wake, #BrunaBiancardi wanadaiwa kuwa wametengana mwezi mmoja tu baada ya kupata mtoto wao wa kwanza.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali inaelezwa kuwa kuwa uamuzi wao wa kutengana umekuja baada ya uvumi katika wiki za hivi karibuni kwamba hawapo tena pamoja, huku kukiwa na tetesi za mchezaji huyo kutokuwa mwaminifu kwa mpenzi wake.

Biancardi mwenye umri wa miaka 29, inadaiwa kuwa amethibitisha kuwa hayupo kwenye mahusiano na nyota huyo na wamebaki kuwa wazazi wa mtoto.

Hata hiyo kuna ripoti zinadai kuwa wawili hao walikuwa na mkataba wa ajabu ambao ulimruhusu Neymar kutaniana na kulala na wanawake wengine kwa masharti maalum ya mkataba ikiwa ni pamoja na Mbrazili huyo hakuruhusiwa kuwabusu wanawake mdomoni na atalazimika kutumia kondomu wakati wa ngono.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 31, anayekipiga katika ‘klabu’ ya #AlHilal SFC ya Saudia, na Biancardi Oktoba 7 walitangaza kumkaribisha binti yao aitwaye Mavie.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags