Kipindupindu chauwa 10, Afrika kusini

Kipindupindu chauwa 10, Afrika kusini

Idara ya afya jimbo la Gauteng kutoka nchini Afrika Kusini siku ya jana Jumapili ilitangaza visa vipya 19 vya Kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo 10, katika mji wa Hamman-skraal. 

Iliripotiwa kifo cha kwanza kilichotokana na kipindupindu mwezi Februari mwaka huu baada ya wagonjwa waliokuwa na virusi hivyo, kuwasili kutoka nchini Malawi.

Lakini haikubainika wazi ni wagonjwa wangapi wa kipindupindu walioko nchini kote ila jimbo hilo lenye watu wengi zaidi la Gauteng ndilo lililoathirika zaidi.

Ikumbukwe mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo ulishuhudiwa kati ya mwaka 2008 na 2009, wakati ambapo takriban visa 12,000 viliripotiwa, kufuatia mlipuko katika nchi jirani ya Zimbabwe.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post