Kipa wa jana Stars atoa neno

Kipa wa jana Stars atoa neno

Baada ya Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wageni wao Morocco ‘mechi’ ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa jana Uwanja wa Mkapa, ‘golikipa’ Kawawa atoa neno baada ya ‘mechi’ hiyo.

Mlinda mlango huyo aitwaye Kwesi Kawawa ametoa shukurani kwa kuchaguliwa kucheza katika mchezo huo kwani ni mechi yake ya kwanza ya kimataifa kufuzu kombe la dunia hivyo basi ni matuamaini yake watarudi wakiwa imara.

Kwasi ameeleza kuwa amefurahishwa sana na ‘sapoti’ ya watanzania na amepokea maoni yao na atayafanyia kazi.

Kwasi alikuwa mlinda mlango katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo ambapo mabao ya Morocco yalifungwa na Hakim Ziyech na Lusajo Mwaikenda akijifunga bao la pili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags