Kim Kardashian: Naenjoy kuwa Single

Kim Kardashian: Naenjoy kuwa Single

Mfanyabiashara kutoka Marekani Kim Kardashian amefunguka kuwa kwa sasa hana mpango wa kuingia kwenye mahusiano kwani anaenjoy kuwa single.

Kim ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye kipindi cha ‘The Tonight Show With Jimmy Fallon’ ambapo mtangazaji alimuuliza kuhusiana na maisha yake ya mapenzi, ambapo alidai kuwa kwasasa anafuraha kuwa single licha ya watoto wake North West, (11), Saint West (8), Chicago West (6), na Psalm West 5) kuhangaika kumtafutia mchumba.

Aidha Kim aliweka wazi kuwa watoto wake hao wamekuwa waangalifu kuchagua mtu atakaye mfaa mama yao kwa kutengeneza orodha inayojumuisha wachezaji mpira wa kikapu, soka na watengeneza maudhui mtandaoni.

Lakini kwa sasa ameamua kuwakataza kufanya hivyo kwani sio jambo ambalo analitaka kwenye maisha yake.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Tmz inaeleza kuwa huenda Kim ameamua kupumzika kwenye mahusiano kwani mpaka kufikai sasa ameshapokea talaka 3 kutoka kwa wanaume tofauti akiwemo ‘rapa’ Kanye West.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags