Kim Kardashian amalizana Beckham Jr

Kim Kardashian amalizana Beckham Jr

Mwanamitindo na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani #KimKardashian amedaiwa kuachana na mwanasoka Odell Beckham Jr baada ya kutoonekana naye pamoja hivi karibuni.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tmz News imeeleza kuwa mrembo huyo na nyota wa NFL wamekuwa hawaongozani tena kama ilivyo kuwa awali ingawa haijulikani ni lini waliachana

Wawili hao wamekatisha mahusiano yao waliyoyaanzisha mwaka 2023 na wameamua kuwa marafiki wa kawaida na inadaiwa kuwa mpaka sasa bado wanaheshimiana kama marafiki.

Ikumbukwe kuwa mrembo huyo aliwahi kufunga ndoa na ‘rapa’ Kanye West mwaka 2014 na kupeana talaka mwaka 2022 pia wamebahatika kupata watoto wanne #North, #Saint, #Chicago na #Psalm.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags