Kim azua taharuki kwenye mtandao wa X, picha aliyochora mwanaye yamponza

Kim azua taharuki kwenye mtandao wa X, picha aliyochora mwanaye yamponza

Mfanyabiashara na mwanamitindo Kim Kardashian ajikuta akizua taharuki na kuitwa muongo kwenye mtandao wa X,baada ya ku-post mchoro unaoonesha machweo ya jua na kudai kuwa mchoro huo ameuchora mtoto wake North West.

Kufuatia ubora na uzuri wa mchoro huo wengi wamejikuta wakikataa na kumtupia maneno ya kuwa aache udanganyifu kwenye mitandao kwani hakuna hata siku moja aliyowahi kuonesha mtoto wake huyo akiwa anaanza hatua ya kwanza ya uchoraj badala yake huwa ana-post picha iliyo kamilika na kudai kuwa mwanaye amechora.

Hii si mara ya kwanza kwa Kim ku-post picha ya mchoro na kudai kuwa mtoto wake ndiye amechora, licha ya wengi kubisha kuwa anadanganya na kudai kuwa wanataka kuona video inayomuonesha mtoto huyo akiwa kwenye hatua ya kwanza ya uchoraji, Kim ameonekana kukaa kimya na kupuuzia maneno ya mashabiki kwenye mitandao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags