Killy: nilisaini mkataba bila mwanasheria

Killy: nilisaini mkataba bila mwanasheria

 Na Asha Charles

Bwana bwana huko mtandaoni leo kumedamshi sio powa, msanii wa bongo fleva kutoka nchini Tanzania Killytz ameongea mazito kuhusiana na mkataba wake na lebo ya Kondegang ambapo alizua maswali mengi kwa mashabiki kuhusiana na alicho kijibu.

Msanii huyo ameeleza kuwa kipindi anasaini Mkataba na Lebo hiyo hakuwa na Mwanasheria na kipindi hicho alikuwa kwenye hali ambayo kijana yeyote Angesaini tu yaani alikuwa katika hali ngumu kimaisha.

“Kiukweli kipindi naingia mkataba na Lebo sikuwa na Mwanasheria na nilikuwa na hali ambayo kijana yeyote angesaini kwa sababu ndio kipindi nimetoka kings Music kwahiyo nilikuwa kwenye hali ambayo sio nzuri, Pengine ningeshirikiana na Mwanasheria nisinge Sign lakini Mungu ndio anajua huenda nilipita ili nijifunze” alisema Killytz

Basi bwana unaambiwa moja ya vipengele katika mkataba huo ambacho msanii huyo alikiweka wazi ni kwamba kama msanii akivunja Mkataba na Lebo atatakiwa kulipa Tsh. Bilioni 1 na Lebo ikivunja Mkataba na Msanii itatakiwa imlipe Tsh. Milioni 10

Oooooh! Naona kama mafuta yashaanza kutengana na maji vile, haya mwanangusana dondosha komenti yako hapo chini kutueleza mtanzamo wako katika hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags