Kijana miaka 18 achaguliwa Meya Marekani

Kijana miaka 18 achaguliwa Meya Marekani

Mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 18 katika jimbo la Arkansas ameripotiwa kuwa meya mwenye umri mdogo kuchaguliwa nchini Marekani.

Siku ya Jumanne, alipigiwa kura kuongoza mji wa mashambani wa Earle, maili 30 (48km) magharibi mwa Memphis, Tennessee.

Familia yake ilishindwa kujizuia kusherehekea ushindi huo mkubwa.

"Mama yangu hawezi kuacha kulia," Bw Smith aliambia Washington Post siku ya Jumatano.

"Ni Wakati wa Kuijenga Earle, Arkansas," Bw Smith aliandika kwenye Facebook kusherehekea ushindi wake.

Akiwa katika shule aliwahi kuwa rais wa chama cha serikali ya wanafunzi wa shule hiyo, na alikuwa na majukumu ya uongozi katika vilabu vya shule.

"Lazima uanzie mahali fulani - kweli ni lazima," aliiambia Post. "Sikutaka kuwa na miaka 30 au 40 na kuwa meya wakati ningeweza kuwa meya hivi sasa."

Bw Smith anapanga kuendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Arkansas Mid-South anaposhughulikia majukumu yake ya umeya.

Smith si meya wa kwanza mwenye umri wa miaka 18 katika historia ya Marekani, Mwaka 2005, Michael Sessions mwenye umri wa miaka 18 alishinda umeya wa mji wa Hillsdale, Michigan kabla hata hajamaliza shule ya sekondari.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags